Monday, May 17, 2010

UPAPARAZI SI KAZI YA LELEMAMA!

Upaparazi shurti kwa vipimo...lengo!...upate picha yenye kiwango!!

Wadau, hii sio sarakasi...Paparazi wapo kazini!..
***

SPOTI
Tenis
Rafael Nadal am'bwaga mpinzani wake Roger Federer ktk mchezo wa fainali wa Madrid Open. Nadal alishinda kwa seti: 6 - 4; 7 - 6; 7 - 5 na kuwa Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2010. Huu ni ushindi wa 168 kati ya michezo 174 aliyocheza tokea mwaka 2005. Kwa ushindi huu Nadal ameendelea kushika namba 2 kwa ubora, nyuma ya Federer.
Rafael Nadal akishangilia ushindi wake

dhidi ya Roger Federer ktk fainali ya Madrid Open

***

SEKESEKE LA MOSHI WA VOLCANO HUKO ULAYA
Hali ya sintofahamu inaendelea kuzitesa nchi nyingi za bara Uropa kutokana na kuendelea kuwepo kwa moshi mkubwa unaosababishwa na mlipuko wa volkano ya mlima.... Hali hii imetatiza safari za ndege barani humo na kuacha mamia ya ndege kukatisha ratiba za usafiri kwa sababu za kiusalama. Mdau, hali ni tete, hebu jionee mwenyewe picha chache za moshi huo hapa chini:

***

No comments:

Post a Comment